Serikali ya Uganda imeanza kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na mlipuko wa homa ya bonde la ufa pamoja na ile ya homa ya Kongo.
Wizara ya afya inasema hadi sasa ni watu wanne ndio wanajulikana kufariki kutokana na mlipuko huo uliotokea katika wilaya za Luwero na Nakaseke kilomita 70 na ushei kaskazini mwa mji mkuu wa Kampala.
Waziri kutoka wizara ya afya anaehusika na masuala ya jumla Sarah Opendi ameiambia Radio ya UN kuwa kuna mpango wa kuua kupe wakitumia dawa mpya ya kunyunyuzia mifugo katika maeneo hayo.
Waziri afafanua jinsi homa hizo jinsi zinavyoambukiza akieleza kuwa chanzo ni mdudu aina ya kupe.
Muwakilishi wa shirika la afya dunini WHO nchini humo, Dr Yonas Tegegn kupitia taarifa amesema kuwa Uganda kama taifa lililotia sahihi kanuni za kimataifa za afya imefuata vilivyo masharti ya kutoa taarifa kuhusu visa vya homa ya bonde la ufa pamoja na ile ilipewa jina la homa ya kongo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni