Jumatatu, 8 Januari 2018

Taarifa iliyoripotiwa kuhusu kuungua kwa jengo la Trump Tower

January 8, 2018 Maafisa wa kuzima moto wameitwa katika jengo linalomilikiwa na President Donald Trump la Trump Tower katika kisiwa cha Manhattan jijini New York kwa ajili ya kuzima moto ambao umezuka kwenye ghorofa ya juu ya jengo hilo.
Idara ya zima moto ya New York imesema moto huo umedhibitiwa na hakukuwa na majeruhi. Shirika la habari la CBS News limesema moto huo ulizuka  saa moja asubuhi  kwa saa za Marekani kwa huku ni saa sita mchana, karibu na paa la jengo hilo la ghorofa 68.
Jumba hilo lilikuwa makazi rasmi ya Bw Trump kabla ya kuapishwa kuwa Rais wa Marekani mwaka mmoja uliopita.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni