
Mbunge wa Chalinze kupitia Chama cha Mpainduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete
amekanusha ujumbe unaosambazwa katika mitandao ya kijamii ukidai kuwa
amekikosoa chama hicho kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wake.
Akizungumza jana jioni, Ridhiwani amewataka watanzania na wanachama wa
CCM kupuuza taarifa hiyo kwani siyo yeye ameitoa na badala yake ni watu
wenye lengo lakukiharibu chama hicho.
Amesema kwamba, kwa siku nzima ya jana hajaandika ujumbe wowote na
kwamba alikuwa jimbo kwake katika vikao vya halmashauri wakipanga
mipango ya bajeti kwa ajili ya maendeleo ya jimbo hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni