
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameanika madudu mengine ya Wizara ya Madini akisema kuwa baadhi ya wateule wake katika wizara hiyo wamekuwa wazembe katika kutekeleza maagizo na kutimiza majukumu yao kama watendaji wa serikali.
Magufuli
ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akimwapisha Mhe. Dotto Mashaka
Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
ametolea mfano wa sheria mpya ya madini iliyopitishwa bungeni mwezi
Julai mwaka jana, ambapo amesema mpaka sasa wizara hiyo haijapitisha
kanuni (regulations) ili sheria hiyo iweze kufanya kazi jambo ambalo
amesema ni uzembe usiovumilika huku akimwagiza Waziri wa Sheria, Prof.
Palamagamba Kabudi kukamilisha kanuni hizo na kuzisaini kufikia Ijumaa
ya wiki hii.
“Nakushukuru
Mhe spika kwa kutoa ushauri kwa serikali na sisi tumekuwa tukiufuata
sana. Wizara ya madini ina changamoto sana na hata sasa ina changamoto
na haifanyi kazi vizuri. Spika utakumbuka mwezi wa saba mlifanya
marekebisho ya sheria ya madini.
"
Na ilipokuja kwa kwangu siku hiyo hiyo nilisaini na kuipitisha, lakini
tangu Julai mpaka sasa regulations (kanuni) hazijasainiwa lakini sheria
imepitishwa na bunge, hivyo sisi Watanzania watumishi hatupo serious.
“Nasikitika
kusema baadhi ya ninaowateua hawajajua nataka nini. Ndiyo maana
nikamteua aliyekuwa kwenye kamati ya madini, labda atatoa changamoto kwa
wenzake maana huenda yeye anaelewa zaidi.
"Na
mnada wa Tanzanite hautafanyika tena mpaka regulations zitakaposainiwa.
Sasa mpo manaibu wawili na waziri wa sheria yupo hapa nataka
regulations hizi zisainiwe kabla ya Ijumaa, tumeibiwa mno, sasa nimesema
imetosha,” alisema Rais Magufuli kwa uchungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni