Jumanne, 2 Januari 2018

MWANZO NA MWISHO WA MAISHA YA FRANCO LUAMBO LUANZO MAKIADI

Image result for franco luambo images







Image result for franco luambo images

 

KUMBUKUMBU YA FRANCO LWANZO MAKIADI

François Luambo Luanzo Makiadi  alizaliwa 6 July 1938, katika kijiji cha Soni Bata magharibi mwa jimbo la Bas Zaire huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Wakati bado mchanga wazazi wake walihamia jiji la Leopodville ambalo sasa linaitwa Kinshasa. Baba yake aliitwa Joseph Emongo alikuwa mfanyakazi wa shirika la reli wakati huo mama yake alikuwa akiuza maandazi sokoni. Alipofikia umri wa miaka saba alitengeza gitaa lake akawa analipiga kwenye genge la mama yake ili kuita wateja.. Mwanamuziki maarufu Paul Ebengo Dewayon ndie aliyegundua kipaji cha mtoto huyu na kuanza kumfundisha rasmi namna ya kupiga gitaa. Mwaka 1950 akiwa na umri mdogo wa miaka 12 alichukuliwa rasmi kama mwanamuziki wa bendi ya Watam iliyokuwa inaongozwa na Dewayon. Kipaji chake kiliwashangaza wengi hasa kwa vile alikuwa akionekana umbo lake kubwa kama gitaa analolipiga lakini akiwa analipiga kwa umakini mkubwa. Akiwa na miaka 15 alirekodi nyimbo yake ya kwanza Bolingo na ngai na Beatrice (Mapenzi yangu kwa Beatrice). Wimbo huu aliutunga alipojiunga na bendi iliyokuwa inamilikiwa na Studio za Loningisa. Kiongozi wa bendi hiyo Henri Bowane ndie aliyeanza kufupisha jina la mwanamuziki huyu na kumuita Franco, jina alilokuja kujulikana nalo maisha yake yote. Mwaka 1955 alianzisha bendi akishirikiana na Jean Serge Essous bendi ilizinduliwa katika ukumbi wa OK Bar, hatimae bendi ilichukua jina la OK Jazz kwa heshima ya bar ambapo ilizinduliwa.Katika muda mfupi ikiwa na mwimbaji Vicky Longomba(Baba yake Lovy Longomba) walianza kuwa bendi pinzani ya bendi kongwe ya African Jazz iliyokuwa inaongozwa na Grand Kalle. Mwaka 1958 Essous na Franco kuwa kiongozi na mtunzi mkuu wa kikundi alichokuja kukijenga kwa kuanzia watu 6 hadi kufikia  watu 30 kwenye mwaka 1980. Franco mwenyewe alikuwa anasema OK Jazz iliweza kutoa album 150 katika miaka 30 ya bendi hiyo.Mwaka 1958 Franco alifungwa kwa mara ya kwanza kwa kosa la uendeshaji mbaya wa gari siku ya kutoka kwake jela ilikuwa kama shujaa katoka vitani. 1960 Vicky Longomba aliacha bendi. Lakini wakati huo Kongo ilikuwa kwenye vuguvugu za kutafuta uhuru na nchi ilikuwa si shwari Franco akahamia Ubelgiji. Baada ya Mobutu Sese Seko kushika nchi na kukawa na amani  katika nchi iliyoitwa sasa Zaire franco alirudi 1966. Akashiriki katika Tamasha la Sanaa Za Afrika lililofanyika Kinshasa 1966 na Franco akawa kipenzi cha serikali ya Mobutu. 
Franco hakuwa tu mwanamuziki mzuri bali pia aliendesha vizuri sana biashara zake za kurekodi na kampuni alizozianzisha wakati huo. Alikuwa na lebo kama (Surboum OK Jazz, Epanza Makita, Boma Bango and Éditions Populaires). Katika miaka ya 70 muziki wa Kongo ulishika kasi sana Afrika na Franco akiongoza jahazi kwa nyimbo kama Infidelité Mado,  na akaendeleza kupiga mitindo mbalimbali kama Bolelo na muziki uliotokana na ngoma za asili toka Kongo zikichanganywa na mapigo kutoka Cuba na kuanza upigaji wa gitaa uliokuja itwa Sebene.
 Mwaka 1970 Franco alimpoteza mdogo wake ambaye nae alikuwa mpiga gitaa mashuhuri Bavon Marie-Marie Siongo ambaye alifariki katika ajali ya gari baada ya kuwa akiendesha gari kwa hasira baada ya ugomvi na kaka yake wakigombea msichana ambaye nae alipata kilema kutokana na ajali hiyo. Lilikuwa pigo kubwa kwa Franco kwa miezi kadhaa aliaacha hata kupiga muziki. Baada ya hapo OK Jazz ilibadili jina na sasa kuitwa TP OK Jazz na mwaka 1973 kutoa kibao kingine kilichotikisa Afrika ,AZDA.  Wimbo huu kwanza ulirekodiwa kama tangazo kwa ajili ya  kampuni ya Volkswagen VW. Mahusiano yake na Mobutu yalikuwa na mawimbi mara wakipatana mara wakikosana kutokana na Franco kuwa anatumia nyimbo zake kukosoa serikali ya Mobutu. 1970 Franco alikuwa ni Rais wa wanamuziki wa Kongo na pia kuajiliwa na kampuni ya kugawa mirabaha ya wanamuziki. Aliendelea kutajirika kwa kuweza hata kunua ardhi nchini Ufaransa, Ubergiji na Kongo, na kuwa na nightclub 4 kubwa kuliko zote Kinshasa kwa wakati huo na kufanya club ya
 Kuwa ndio makao makuu yake. Hapo ilijengwa studio kubwa, office na apartment za kuishi kadhaa. Mwaka 1978 alitiwa mbaroni  tena baada ya kugundulika kuwa alikuwa anasambaza nyimbo zenye matusi ambazo hakuzipitisha katika  kamati ya kuchunguza mashahiri kama ilivyokuwa kawaida wakati ule. Kufikia kipindi hiki TPOK Jazz  ilikuwa kubwa kiasi iliweza kumeguka kuwa mbili moja ikifanya kazi Afrika wakati nyingine ikiwa inafanya maonyesho Ulaya. !983 Franco alifanya maonyesho kadhaa Marekani lakini hayakufanikiwa haijajulikana mpaka leo sababu za kushindikana huko. Katikati ya miaka ya 70 Franco alibadili dini na kuwa Muislam na kupewa jina la Abubakkar Siddiki, japo hakuonekana kufuata taratibu zozote za Kiislamu na akaendelea kuitwa Franco. 1980, Franco alitajwa kama ndie Grand Master wa muziki wa Kongo na serikali yake, ghafla na nyimbo zake nyingi zikaanza kuwa zinasifia utawala ulikuweko madarakani. 1985 Franco alitoa wimbo ambao uliuza kuliko nyimbo zake zote
, Mario,  ambao ulikuwa ni hadithi ya mwanaume kijana  ambae alikuwa anategemea akina mama watu wazima wamlee. !987 zilianza habari kuwa Franco anaumwa sana, na kwa mwaka ule alitoa wimbo mmoja Attention Na SIDA
 
 (Jihadhari na UKIMWI), wimbo huu ukaanzisha maneno kuwa pengine Franco kasha upata ugonjwa huu. Franco akawa taratibu anakosekana kwenye shughuli za bendi nayo ikaanza kumeguka kutokana na kutokuwa na uongozi thabiti. Franco tena akarudi kwenye dini yake ya awali ya Roman Catholic. Tarehe 12 Oktoba 1989, Franco alifariki katika hospitali moja Ubelgiji. Mwili wake ukarudishwa Kongo, sanduku likiwa limefunikwa bendera ya Taifa lake na kupitishwa katika mitaa ya Kinshasa na kuagwa na maelfu ya wapenzi wake. Serikali ikatangaza siku 4 za maombolezo ambapo redio ya serikali ilipiga nyimbo za Franco tu. Franco alizikwa tarehe17 Oktoba 1989. Alifariki akiwa na miaka 51. Mumgu amlaze pema pepon




















bbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbbb
Franco ambaye alizaliwa Tarehe 6 Julai, 1938, katika Kijiji cha Sona Bata Magharibi ya Kongo, atakumbukwa na watanzania wakati alipofanya onyesho kweye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwaka 1973.

Baba yake Joseph Emogo alikuwa mfanyakazi wa Shirika la reli wakati mama yake alikuwa mama wa nyumbani akioka mikate na kuuza Sokoni wakati akiwa bado mdogo wazazi wake walihamia katika Jiji la Kinshasa.
.

Franco alipofikisha umri wa miaka Saba alitengeneza gitaa la kienyeji ambalo alilitumia kupiga na akiwavutia wateja pembeni  mwa mama yake wakati akiuza mikate.

Kipaji chake kiligunduliwa na mpiga gita Paul Ebengo Dewayon ambaye alijitolea kumfunza Franco jinsi ya kupiga vyema Ala hiyo.

Mwaka 1950, wakati huo akiwa na umri wa miaka 12, alitengeneza jina akiwa katika bendi ya Watam ya Ebengo Dewayon ambaye alikuwa kiongozi wa bendi hiyo.

Alizikonga nyoyo za wapenzi  kwa uwezo wakemkubwa wa kupiga gita ambalo lilikuwa kubwa kuliko yeye.Miaka mitatu baadaye Franco alirekodi  wimbo wake wa kwanza uliokuwa na jina la Bolingo na Ngai na Beatrice.(mpenzi wangu Beatrice) baada ya kukubalika kuwa mmoja wa wana bendi ya Loningisa Studio, kiongozi wa bendi hiyo Henri Bowane alitoa nadhiri kwamba ataishi na Franco katika maisha yake yote yaliyosalia.

Chini ya Henri Bowane Franco akawa mpiga gita la solo ambapo alikuwa kipiga staili ya Sebene  na akaanza kutunga na kuimba yeye mwenyewe kwa staili za rumba na za kiafrika na hata za kilatini.

Mwaka 1955 pamoja na kwamba alikuwa akipewa kazi nyingi katika Studio hapo Franco aliunda bendi akiwa na Jean Serge Essous iliyokuwa ikipigia katika Baa ya Ok.

Huko Kinshasa.
Mwaka uliofuatia bendi hiyo ilibadilishwa jina na kuwa Ok Jazz na baadaye ikaitwa T.P.Ok. Jazz kuenzi sehemu ilipoanzia bendi hiyo yaani katika Bar yenye jila la OK (OK. Bar)

Katika kipindi cha mwaka mmoja bendi yake ya T.P.Ok Jazz ikagundulika kwamba inataka kumpiku Vicky Longomba ambaye alikuwa katika bendi ya Grand Kale ya African Jazz ambayo ndiyo ilikuwa bendi kubwa nchini Kongo.

Franco alishadai kwamba bendi yake ya Ok.Jazz ilitoa zaidi ya album 150 katika kipindi cha miaka 30.
Mwaka 1958  Franco alifungwa kwa kosa la  ajali ya barabarani.

Purukushani za kisiasa katika nchi yake ya Kongo Franco alilazimika kuhamia Ubelgiji kwa ajili ya kurekodi nyimbo zake.

Baada ya nchi kutulia ikiwa chini ya uongozi wa rais Mobutu Seseseko Kuku Ng’endu Wazabanga ambaye alibadilisha jina la Kongo kuwa Zaire, Franco alirudi nchini mwake na kafanya tamasha kambambe la Festival Ok. Jazz f African Arts lililofanyika Kinshasa mwaka 1966.

Ok Jazz iliisaidia sana Serikali ya Mobutu katika mambo ya kisiasa kupitia nyimbo zake zilizokuwa na mafunzo mengi.Franco hakuona soni katika kusifia mazuri wala kuonya mabaya pamoja na kwamba aliwekwa lupango mara nyingi alipokiuka taratibu za nchi.


Mwaka  1970 Franco alipata pigo kubwa kwa kufiwa na mdogo wake  Bavon Marie Marie amabaye kifo chake kilitokana na ajali ya gari alipokuwa akiendesha kwa hasira baada ya kukorofishana na kaka yake Franco juu ya mwanamke ambaye pia alikufa katika ajali hiyo.

 Mwaka 1980 Serikali ya Kongo (Zaire) ilimtunuka hadhi ya kuwa Babu wa muziki wa Kongo kama heshima kwa juhudi zake za kufufua uchumi amabo ulikuwa ukiyumba nchini humo.

Wakati wa maisha yake aliwahi kuongeza uzito ghafla na kufikia paundi 300 ambazo ni sawa na kilo 136.
Franco alifyatua wimbo mkali mwaka 1985, uliotikisa nchi wa Mario. Lakini mwaka 1987 fununu zikaanza kuzagaa kwamba Franco yu mgonjwa.

Wimbo aliotengeneza mwaka huo kabla ya kifo chake ulikuwa wa ‘Attention na SIDA’(Jihadhari kwa Ukimwi / AIDS)
Franco alifariki tarehe 12, Oktoba 1989 akiwa katika hospitali mojawapo huko Ubelgiji na mwili wake ulisafirishwa kupelekwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Zaire zamani) ambako jeneza lake lilipitishwa mitaani kuagwa na wananchi likisindikizwa na ulinzi mkali wa Polisi na baadaye serikali ikatangaza siku nne za maombolezo ya kitaifa.

Wakati wa siku hizo za maombolezo radio ya taifa hilo ilikuwa ikipiga nyimbo za Franco hadi tarehe 17, Oktoba 1989  alipozikwa kwa heshima zote za kitaifa.


TUMKUMBUKE GRAND MAITRE LUAMBO MAKIADI / NYIMBO ZAKE ZILIZO PIGWA MARUFUKU

 

Miaka 25 Sasa tokea Afariki Dunia Guiji wa Muziki wa Rumba FRANCO LUAMBO MAKIADI.
Ingawa Mengi yamesha andikwa kwa kumhenzi GRAND MAITRE FRANCO, Leo hii nachukua fursa ya kuchambua Baadhi ya Nyimbo zake zilizo pigwa Marufuku.
Wala sio Siri tunapo tamka ya kwamba ” GRAND MAITRE LUAMBO MAKIADI FRANCO ” katokea kua Tajiri sana katika kipindi cha Utawala wa Rais MOBUTU SESESEKO.
Mbali na Urafiki ambao FRANCO LUAMBO alikuanao na RAIS MOBUTU, ilifikia wakati fulani Serekali ikazipiga marufuku Baadhi ya Nyimbo zake zilizo kua na Ujumbe uliokeuka Maadili ya Umma.
Kutokana pia na Sababu mbali mbali, SEREKALI YA RAIS MOBUTU, ilikua makini sana na Wanamuziki, hasa palikua na Watu hodari ambao kazi yao kuu ilikua kufanya uchunguzi wakina kwa Ujumbe unao patikana kwenye NYIMBO. Ikiwa kwa Namna moja au Nyingine kwenye Wimbo wewe Msanii ukithubutu Kutamka Jina la Mpinzani, Basi Wimbo huo kamwe hauta ruhusiwa na Wewe mwenyewe utajikuta ukiwa matatani.
1. Mkasa kama huo umemkuta  TABU LEY ROCHEREAU, wakati katunga Wimbo ” KASHAMA NKOYI ” kwenye Wimbo huo, ROCHEREAU kayatamka Maneno haya : ” Boni Oweleli, Okende liboso ya Baninga, Soki okutani na LUMUMBA okoloba nini PAPA ?  Tokengelaki yoo te  KASHAMA  NKOYI / INAKUAJE UKASAFIRI, WATUTANGULIA SISI WENZIO, HUKO UENDAKO, UTAKAPO KUTANA NA LUMUMBA UTAMWAMBIAJE BABA ? WALA HATUJAWAHI KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA KWA YALE YALIYO KUKUTA ” KASHAMA NKOYI “.
Wimbo umepigwa Marufuku, sio kwasababu  Katajwa LUMUMBA hapana, Bali Jina ” KASHAMA NKOYI “, Serekali ya MOBUTU yamushutumu ROCHEREAU TABU LEY kutumia Jina hilo Bandia kwakumhenzi ” PIERRE MULELE ” ambae alikua Mmoja kati ya MAWAZIRI wa EMERY PATRICE LUMUMBA,SHUJAA WA UHURU WA CONGO. Baada ya kuuwawa LUMUMBA, PIERRE MULELE kasimama kidete kupambana na SEREKALI ya MOBUTU. Vikosi vya Waasi vilio tawala mashariki mwa Congo hasa kwenye Mikoa ya KIVU. VIlikua vikimchukulia yeye kama Kiongozi wao Mkuu. Ndiko katokea LAURENT DESIRE KABILA. PIERRE MULELE kauwawa Mwaka 1968.
2. FRANCO LUAMBO NA WIMBO WAKE ” LUVUMBU NDOKI “, Kwenye Wimbo huo, FRANCO kaimba kwa KIKONGO, Lugha yake ya Asili. Ujumbe kwenye Wimbo huo ni kwamba ” WEWE LUVUMBU MTU AMBAE KIJIJI KIZIMA KINAKUTEGEMEA, WANAKIJIJI WOTE WAKO CHINI YA USIMAMIZI WAKO, KUTOKANA NA UCHAWI WAKO, UMEWAMALIZA NDUGU ZAKO WOTE WAKIKE KAMAVILE WAKIUME, SASA WAKATI UTAKAPO FARIKI, NANI YULE ATAKAE KUZIKA ? MIMI FRANÇOIS NASHINDWA KABISA KULIA, KWAKWELI HUA NAJIULIZA, KWANI UCHAWI WAKO UPO MGONGONI AU TUMBONI MWAKO.
Wimbo huo Ulipigwa marufuku paletuu ulipo tolewa, SEREKALI ya RAIS MOBUTU, yasema kwamba, Kupitia Wimbo huo, FRANCO LUAMBO MAKIADI kawatukuza Wanasiasa Wanne Walio Uwawa kwa Kunyongwa kwa Madai kwamba walikua na nia ya kuipindua Serekali Mwaka 1966.  Wanasiasa hao walio nyongwa ni hawa :
1. JÉRÔME ANANY ( WAZIRI WA ZAMANI WA ULINZI WA TAIFA )
2. EMMANUEL BAMBA ( SENETA )
3. ÉVARISTE KIMBA ( WAZIRI MKUU WA ZAMANI )
4. ALEXANDRE MAHAMBA ( WAZIRI WA ARDHI )
Baada ya Wimbo huo kutolewa, FRANCO LUAMBO  Tetesi zilimjia kana kwamba SEREKALI ipo kwenye harakati ya kumfungulia Mashitaka na Kumuweka Jela. LUAMBO kavuka yeye pamoja na Group lake nakwenda kujihifadhi kwa Mda JIJINI BRAZZAVILLE.
Akiwa JIJINI BRAZZAVILLE, RAIS MOBUTU kamtumia Wajumbe na kumshawishi arudi KINSHASA, maisha yake haitakua hatarini. FRANCO LUAMBO kaupokea wito huo ila kawa katika hali ya Mtu mwenye Kusita. Mwishowe kaamua kurudi KINSHASA.
Akiwa JIJINI KINSHASA, FRANCO LUAMBO kajikuta yuko matatani, Kakaribishwa na kikosi cha Wanajeshi. Wakamuamuru yeye na Group lake wapande ndani ya Gari lao, nakupelekwa moja kwa moja  Jela ya NDOLO. Huko walikaa kwa Mda wa Siku Mbili, yasemekana Walicharazwa bakora sawasawa,
Baada yakutolewa kwenye Jela ya NDOLO,  FRANCO LUAMBO na Group lake, wakahamishwa kwenye Kambi ya Jeshi ” TSHATSHI “. Huko pia wakashikiliwa kwa siku kadhaa wakiwa kambini humo.
Ndipo Ikatokea Siku amabayo RAIS MOBUTU akaja mwenyewe kujadiliana na LUAMBO MAKIADI. kamtamkia Maneno haya : ( KUANZIA LEO HII HADI ITAKAPO FIKIA WAKATI WA MIMI KUONDOKA MADARAKANI, UTAKUA UKINIIMBIA MIMI, WATAKIWA KUNIFANYIA KAZI ZANGU ZOTE, NA TENA KWA WAKATI WOWOTE NTAKAO KUHITAJI ) .
Nakwakeli Tokea siku hiyo, FRANCO LUAMBO kawa kiungo kikuu sana kwa Kampeni ya RAIS MOBUTU. na kutokana na ushirikiano huo, kanufaika sana kuwazidi Wanamuziki wengine wote wa Inchi hiyo katika kipindi hicho cha utawala wa Serekali ya MOBUTU SESESEKO KUKU NGBWENDU WAZABANGA JOSEPH DESIRE.
Mwaka 1978,  FRANCO LUAMBO MAKIADI kawekwa tena JELA kutokana na Utunzi wa Nyimbo ( HELEINI na JACKIE ),
Nyimbo mbili hizo zilikua na Maneno machafu sana tena yaku yaharibu maadili ya Umma. Sheria ikachukuliwa kuzipiga Marufuku zisipitishwe kwenye Radio na TV ya taifa. FRANCO mwenyewe kajitetea, kasema wala NYIMBO hizo hajizauzwa Sokoni zilikua bado hazijawekwa kwenye CD. bali Watu walikua wakizisikiliza Wakati wa SHOO kwenye Ukumbi wake wa 1.2.3 KINSHASA.
Aliekua MWANASHERIA MKUU WA SEREKALI kipindi hicho  ” Mr  LEON KENGO WA DONDO “,kalisimamia swala hilo, nakuamuru FRANCO LUAMBO awekwe Jela, kapelekwa kwenye JELA ya ” LUZUBU ” inayo patikana kwenye MKOA WA BAS CONGO aliko zaliwa FRANCO.
Huko JELA, FRANCO kawa mwenye masikitiko, Kwanini RAIS MOBUTU kashindwa kumsaidia ? yeye ambae alikua akimchukulia kama Rafiki. FRANCO kapigwa na Ugonjwa wa HEMORRHOID. katabaanika kabisa. Kabaki na chuki na kinyongo dhidi ya MWANASHERIA ” LEON KENGO WA DONDO ” aliempeleka JELA. Haelewi kwanini kawekwa kizuizini wakati Hajawahi kuzidumbwiza Nyimbo hizo hadharani.
Miaka michache baadae, palitokea na mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri, LEON KENGO WA DONDO  Kanenguliwa Cheo cha MWANA SHERIA MKUU WA SEREKALI na kutomwa JIJINI BRUSSELS kama BALOZI WA CONGO.
Furaha ilikuaje kwa FRANCO LUAMBO MAKIADI ?, bila kukawia kamtungia Wimbo ” TAILLEUR ” kwenye Wimbo huo FRANCO kanena haya : ( LIKAMBO NALOBAKI LOBI, MONOKO NA NGAI NGANGA / UTABIRI WANGU WATOKEA KUA KWELI, MDOMO WANGU KAMA WA MGANGA WA JADI ).
MOKOLO TONGA ABOTOLI TONGA OKOTONGA NANI ? / MWENYE SINDANO YAKE KESHA ICHUKUA, SASA UTATUMIA NINI ILIUENDELEE KUWACHOMA WENGINE?
OLOBAKI TROP NA ESIKA YANGOO BATIE YO PEMBENI LOBA LISUSU MAMA / ULIKUA UKIKIJIVUNIA SANA CHEO HICHO, SIUMEONA WAMEKUONDOA, UNANINI CHAKUONGEA? Wimbo huo pia ukapigwa Marufuku kwa Mda.
Mwaka 1982, RAIS MOBUTU Kamwitisha LEON KENGO WA DONDO , na kamteua kama WAZIRI MKUU WA INCHI.
FRANCO LUAMBO hajaridhishwa ni kitendo cha RAIS MOBUTU kumpa KENGO WA DONDO cheo cha WAZIRI MKUU, bila kusita Katunga Wimbo ” TRES FACHE “. Mtamsikia akiiimba : ( OKOSI NGAI MAMA YONAYE BOBOYANA, LOBI LISUSU BAKUTI YO NA VOITURE NA YEE, ELOKO NASALA NAYEBI TEEOO MOKILI / WANIDANGANYA KAMA NYIE WAWILI SIO TENA MARAFIKI, KESHO YAKE WATU WAMEWAONA MKIWA PAMOJA NDANI YA GARI, JAMANI KOSA GANI NILILOLIFANYA MIE!!! ). Kadhalika Wimbo huo Ulipigwa pia Marufuku.
GRAND MAITRE LUAMBO MAKIADI KAFARIKI DUNIA  INCHINI BELGIUM TAREHE  12-10-1989.
SIKU YA MAZISHI YAKE, LEON KENGO WA DONDO AMBAE NDIE ALIEKUA WAZIRI MKUU, KAJA KUTOA HESHIMA ZAKE ZA MWISHO KWA NIABA YA SEREKALI.
WAKATI WA MISA  YA MAZISHI YAKE, PADRE KASEMA : ” LUAMBO ALIKUA MTUME WA MUZIKI, HAKUNA ALICHOKISAHAU KATIKA UTUNZI WAKE, KAVICHAMBUA VITU KADHALIKA NA WATU WAKILA RIKA, HATA RAIS MOBUTU HAJAACHWA NYUMA.
NYIMBO ZAKE KADHAA ZILIPIGWA MARUFUKU, HATA HIVYO ZILIENDELEA KUPENDWA SANA NA UMMA. HUKU NYIMBO ZAKE  NYINGINE HADI LEO HUCHUKULIWA KAMA NEMBO YA TAIFA.

  mengineyo kumuhusu franco

 

MIAKA 25 iliyopita, Alhamisi ya tarehe kama ya leo (yaani Oktoba 12, 1989) majira ya saa 1 asubuhi ndipo niliposikia taarifa kupitia BBC kwamba mwanamuziki nguli wa rhumba barani Afrika, Franco, alikuwa amefariki dunia.
Franco alifariki wakati akitibiwa katika hospitali moja jijini Brusells, Ubelgiji, tena alifariki mbele ya dada yake Marie Louise, mkewe Annie baadhi ya wanawe na baadhi ya wanamuziki wa bendi yake.
Zile fununu zilizokuwa zimeenea tangu mwaka 1987 kwamba nguli huyo alikuwa anaumwa sasa zikachukua sura mpya baada ya watu kuanza kuvumisha kwamba huenda maradhi ya Ukimwi ndiyo yaliyokuwa yamekatisha uhai wake.
Hii ilitokana na sababu mbili: kwanza, tangu mwaka 1987 zilipovuma habari hizo kwamba jamaa anaumwa baadaye akaanza kutoonekana mara kwa mara jukwaani. Lakini pili ni baada ya kutoa albam yake – ya mwisho akiwa hai – ya Attention na SIDA (Jihadhari na Ukimwi) mwaka 1987 ambayo kwa hakika hata taasisi za afya za kimataifa, hususan zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi, zinastahili kumuenzi hata leo.
Siyo ajabu kutokea kwa madai hayo, kwa sababu siri ya mgonjwa anaijua mgonjwa mwenyewe na daktari, labda wawili hao waamue kuitoa hadharani. Lakini ni jambo la kawaida hata sasa kwa binadamu kujifanya madaktari – mabingwa wa kupima homa kwa viganja – ambapo wakimuona mtu kakonda kidogo utawasikia wakisema “Yule, aah tayari ana ngwengwe!”
Franco mwenyewe katika kibao cha Attention na SIDA anaimba hivi: “Moto azua malade balobi Sida, moto azua fevre balobi Sida, moto akonda balobi Sida, moto akufa balobi akufi na Sida…” (Mtu akiugua wanasema anaumwa Ukimwi, Mtu akiwa na homa wanasema Ukimwi, mtu akikonda tu wanasema ana Ukimwi, Mtu akifa wanasema amekufa kwa Ukimwi). Upo hapo mjomba!?
Kwa vyovyote vile, dunia ilikuwa imempoteza mwanamuziki ambaye alileta mabadiliko makubwa ya muziki wa Afrika ukakubalika ulimwenguni kote.
Watanzania, hasa wale vijana wa zamani, watamkumbuka kutokana na onyesho kubwa alilolifanya pale kwenye Uwanja wa Taifa (Shamba la Bibi) jijini Dar es Salaam mwaka 1973.
Alipozaliwa Julai 6, 1938 katika Kijiji cha Sona Bata, katika Jimbo la Bas Congo magharibi mwa Congo, si baba yake Joseph Emogo wala mama yake …. waliojua kama mtoto huyo aliyezaliwa njiti angeweza kuja kuwa mtu mashuhuri sana duniani.
Baba yake alikuwa mfanyakazi wa Shirika la Reli enzi hizo za ukoloni wa Mbelgiji wakati mama yake alikuwa akioka mikate na kuiuza sokoni. Mama yake alimpa jina la Makiadi, lakini alipobatizwa kanisani akapewa jina la Francis (ambalo ndilo Franco).
Wakati akiwa mdogo, wazazi wake wakahamia jijini Kinshasa.
Akiwa na umri wa miaka saba tu, Franco alitengeneza gitaa la kienyeji ambalo alilitumia kupiga na kuwavutia wateja pembeni mwa mama yake wakati akiuza mikate na maandazi.
Kipaji chake kiligunduliwa na mpiga gita mashuhuri wa enzi hizo, Paul Ebengo Dewayon, ambaye alijitolea kumfunza Franco jinsi ya kupiga vyema ala hiyo ambayo baadaye ikamfanya aitwe Sorcerer of Guitar (yaani Mchawi wa Gitaa).
Mwaka 1950, akiwa ndiyo kwanza ametimiza miaka 12, Franco alianza kutengeneza jina wakati akiwa na bendi ya Watam iliyokuwa ikiongozwa na Paul Dewayon. Uwezo wake wa kulikung’uta gitaa ulikonga nyoyo za mashabiki wengi ambao walistaajabia umahiri wake wakati umri ukiwa unamsuta.
Miaka mitatu baadaye Franco alirekodi wimbo wake wa kwanza uliokwenda kwa jina la Bolingo na Ngai na Beatrice (Mpenzi wangu Beatrice). Baada ya kukubalika kuwa mmoja wa wana bendi ya Loningisa Studio, kiongozi wa bendi hiyo Henri Bowane alitoa nadhiri kwamba angeishi na Franco katika maisha yake yote yaliyosalia.
Chini ya Henri Bowane, Franco akawa mpiga gita la solo ambapo alikuwa akipiga staili ya Sebene na akaanza kutunga na kuimba yeye mwenyewe kwa staili za rumba, za Kiafrika na hata za Kilatini.
Mnamo Juni 1956 pamoja na kwamba alikuwa akipewa kazi nyingi katika studio, Franco akaamua kuunda bendi akiwa na Jean Serge Essous na De La Lune ambao pia walikuwa wakiimba pale Loningisa Studio. Bendi hii iliyokuwa ikifadhiliwa na mfanyabiashara Omar Kashama wakaipa jina la OK Jazz ambapo ilikuwa ikipigia katika Baa ya OK iliyokuwa ikimilikiwa na mfanyabiashara huyo.
Hapa ndipo kwenye mkanganyiko kuhusu neno OK. Kiasili lilikuwa ni kifupisho cha Omar Kashama, mfadhili wa bendi, lakini baadaye ikajipambanua na herufi hizo zikimaanisha Orchestra Kinois.
Essous alikuwa na kipaji cha upulizaji wa ala kuanzia clarinet hadi saxophone. Wanamuziki wengine waanzilishi walikuwa mpiga bassAugustin Moniania Roitelet, mpiga drums La Monta LiBerlin na Saturnin Pandy, mpiga gitaa Nicolas Bosuma Bakili Dessoin na mwimbaji Philippe Lando Rossignol pamoja na Vicky Longomba.
Bendi hiyo, ikiwa imesheheni vijana wenye vipaji na usongo wa kufanya vizuri kwenye muziki, ghafla ikaanza kuziteka hisia za mashabiki wa muziki nchini Congo. Ilikuwa wazi kwamba hawa jamaa hawakuwa wamedhamiria kupiga muziki wa kujiburudisha, bali kupata mafanikio zaidi wakipiga rhumba lenye kasi siyo kama lile la Africa Jazz ya Joseph Kabaselle ‘Le Grand Kalle’. Kila siku walipiga muziki kwenye studio iliyokuwa ikimilikiwa na Mgiriki mmoja na mara chache wakawa wanatumbuiza kwenye sherehe kama harusi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni