
Jopo la madaktari bingwa wa moyo wa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete limeanza kufanya uchunguzi wa kina wa kuangalia mifumo ya mwili ya watoto mapacha walioungana Consolata Mwakikuti na Maria Mwakikuti baada ya kufikishwa katika taasisi hiyo kutokana katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.
Msemaji wa JKCI Bwana Maulid Kikondo amesema mapacha hao walioungana ambao ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa mwaka wa kwanza wamepolewa katika taasisi majira ya saa tano usiku, ambapo wameanza uchunguzi hususani kwa kuangalia mwingiliano wa mifumo ya damu na moyo ili kubaini tatizo linalowasumbua.
Kwa upande wake mlezi wa watoto wao,Bi Francisca Malangwa amesema Maria alianza ghafla kutapika na kukohoa na kisha tatizo hilo kuamia kwa dada yake Consolata na kulalamika maumivu mwilini na ndipo waliopo wakimbiza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa na kupewa rufaa ya kuja katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kwa uchunguzi zaidi afya zao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni