
Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imesema ililazimika kumtunza faru Fausta kwa kugharamia matibabu ya vidonda alivyo kuwa navyo mwilini mwake pamoja na chakula, kutokana na Umaarufu wa kipekee alionao hii ikiwa ni pamoja na umri wake ambao unakadiriwa kuwa mkubwa kuliko faru wote afrika na pengine duniani.
Faru Fausta Alianza kuhudumiwa rasmi kwa chakula na matibabu ya vidonda mwaka 2016 baada ya Kuanza kushambuliwa na fisi kutokana na uzee hali ambayo ilimsababishia vidonda katika sehemu mbalimbali katika mwili wake.
Aidha kwa mujibu wa meneja wa ekolojia na malisho wa hifadhi hiyo Hillary Mushi, gharama za kumuhudumia faru Fausta zimeendelea kupungua siku hadi siku kutokana na vidonda vyake kunyauka na uanzishwaji wa bustani maalumu ya chakula chake huku mpango wa kuanzisha tozo maalumu ya nyongeza ya kumuona Fausta ukiwekwa wazi.
Aidha katika ziara hiyo Kamati imetembelea pia mradi wa makumbusho mpya ya Olduvai iliyopo ndani ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro ambapo imeonekana kuridhika na uhifadhi wa malikale na visukuku ambavyo hutoa Tafsiri ya chimbuko la mwanadamu wa kwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni