Kwenye mkesha wa kuamkia mwaka mpya wa 2018, moto mkubwa umeharibu zaidi ya magari 1,400 huko nchini Uingereza.
Moto huo ambao ulizuka kwenye jengo la ghorofa la kuegesha magari huko mjini Liverpool uliwalazimu watu waliokuwa wanasherehekea kuupokea mwaka mpya kuamuliwa na Jeshi la Polisi kujifungia majumbani mwao.
Mashuhuda wa tukio hilo kupitia mtandao wa Liverpool Echo wamesema wakati moto unaanza kulipuka kwenye ghorofa hilo walidhani ni baruti za kuukaribisha mwaka mpya lakini baadae wakaona moto mkubwa ukizidi kuenea.
Mamia ya watu waliokuwa wamepaki magari yao kwenye jengo hilo wote wanaeleza kuwa awali wakati moto unazuka hawakujua kama ilikuwa ni ajali walidhani ni baruti.
Tayari mtandao wa Sky News umeripoti kuwa zaidi ya magari 1,400 yameteketea kwenye moto huo na baadhi ya watu waliokuwa wanaishi kwenye Appartment karibu na ghorofa hilo la maegesho la King’s Dock wameokolewa na jeshi la zima moto na hakuna taarifa ya watu kujeruhiwa wala taarifa ya kifo. Tazama video ya tukio hilo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni