
Watabiri wa hali ya hewa wanasema hali
itaendelea kuwa mbaya mashariki mwa Marekani, na tayari kumeanza kuwa na
theluji jimbo la Florida.
Marekani kwa sasa inakumbwa na siku ya 10 ya viwango vya baridi ambavyo vimevunja rekodi majira ya sasa ya baridi.
Baridi kali ilianza wakati wa Krismasi.

dara
ya Taifa ya Utabiri wa hali ya Hewa (NWS) imetahadharisha kwamba hewa
baridi kutoka Arctic itaendelea kutandaza katika theluthi mbili ya
maeneo ya mashariki mwa Marekani hadi mwishoni mwa wiki hii.
Hilo litasababisha wimbi la upepo baridi kama wa kimbunga.
Upepo huo unaweza kuwa na nguvu kiasi cha kung'oa miti na kuharibu majengo.
Viwango vya joto kwa wastani Jumanne maeneo ya mashariki mwa Marekani vilifikia 9.1F (-12.7C) kwa mujibu wa CBS News.
Mji wa Boston ni miongoni mwa miji inayotarajiwa kuathirika pamoja na miji ya mbali kwa mfano Orlando jimbo la Florida.
Wakazi katika maeneo ya kaskazini mwa Florida, ukiwemo mji wa
Tallahassee, wameshuhudia theluji kwa mara ya kwanza katika miongo
mingi.
Wengi wamekuwa wakipiga picha wakicheza kwenye theluji.
Shule katika maeneo mengi zimefungwa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni