Jumapili, 21 Januari 2018

Kundi la Taliban wamevamia hotel ya kifahari Afghanistan







Usiku wa kuamkia January 21, 2018 Watu wenye silaha za kivita  wamevamia hoteli ya Intercontinental katika Mji mkuu wa Afghanistan Kabul na kuwafyatulia risasi wageni na wahudumu wa hoteli hiyo pamoja na kuichoma moto hotel hiyo.
Vikosi vya usalama vimepambana nao kwa zaidi ya saa nane. Naibu waziri wa mambo ya ndani Nasrat Rahimi ameliambia shirika la habari la AFP kwamba washambuliaji wawili kati yao wameuawa.
Hakuna aliyejitokeza kudai kuhusika na shambulio hilo, katika mji mkuu wa Afghanistan ulioharibiwa kwa vita na ambako kumekuwa kukitolewa maonyo ya mfululizo siku za karibuni ya kuwataka watu kuepuka hoteli na maeneo mengine yanayotembelewa na wageni.
Haijulikani watu wangapi bado wamekwama ndani ya hoteli hiyo, ambayo iliwahi kuvamiwa na kundi la Taliban mnamo mwaka 2011, au kama kuna raia wowote wa kigeni miongoni mwao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni