
Kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa amekubali kuwa timu yake
ilizidiwa na Mbao na kujikuta ikiruhusu magoli mawili ndani ya kipindi
cha pili, mlinzi huyo wa zamani wa kulia wa Yanga na Taifa Stars amesema
kipindi cha pili Mbao walibadilika na kutumia nafasi walizozitengeneza
kupata magoli.
Nsajigwa amekubali kuwa Mbao walistahili kushinda mchezo huo baada ya kufanya kazi yao vizuri uwanjani.
“Hali ya mchezo kwa ujumla ilikuwa nzuri kiasi chake, kipindi cha kwanza
mechi ilikuwa nusu kwa nusu lakini kipindi cha pili kilibadilika, Mbao
walibadilika wakaja juu badae wakapata nafasi wakazitumia. Mpira ni
mchezo wa matokeo, usipobadili nafasi ulizopata kuwa magoli basi huezi
kufunga”-Shadrack Nsanjgwa.
“Tumepoteza mchezo tunawapa hongera Mbao wamefanya kazi yao vizuri wamepata ushindi.”
Nsajigwa akishirikiana na benchi la ufundi la Yanga alikiongoza kikosi
kwenye mchezo dhidi ya Mbao bila uwepo wa kocha mkuu George Lwandamina
ambaye yupo kwao (Zambia) ambako amekwenda kuhudhuria msiba wa mtoto
wake aliyefariki hivi karibuni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni