Swala la beki wa klabu ya Kagera Sugar, Juma Said Nyoso kumshambulia shabiki anaesadikika kuwa wa timu ya Simba, Shabani Hussein hadi kuzimia katika mchezo wao wa wiki hii uliyofanyika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba bado halijakwisha licha ya Jeshi la Polisi kumuachia kwa dhamana mchezaji huyo.
Kupitia Mwanaspoti Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Issack Msengi amesema wamemwachia kwadhamana mchezaji Juma Nyoso wakati wakiendelea na upelelezi na ikibainika kuwa ana makosa atafikishwa mahakamani.
Shabiki anaesadikika kuwa wa timu ya Simba, Shabani Hussein ambaye anadaiwa kupigwa na mchezaji Juma Nyoso
“Kuhusu aliyejeruhiwa kwa sasa anaendelea vyema na kesho (leo) tunatarajia kupata ripoti ya kipimo cha Xray alichofanyiwa,” amesema Kamanda Msengi.
Kamanda Issack Msengi ameongeza kuwa wakimuachia Juma Nyoso baada ya kukamilisha taratibu za dhamana na wanaendelea kupeleleza kwa hatua zaidi huku akisema kama itabainika shabiki aliyepigwa alifanya kosa la jinai la kutukana hadharani nayeatafunguliwa kesi juu ya tukio hilo.
Beki huyo wa Kagera Sugar amejikuta akiingia mikononi mwa Jeshi la Polisi hapo juzi baada ya kutuhumiwa kumpiga shabiki na kumzimisha kitendo alichokifanya mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Simba SC uliyomalizika kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya vinara hao wa ligi kuu soka Tanzania Bara.
wakati huohuo Klabu ya Kagera Sugar kupitia kwa Mratibu wake, Mohamed Husein amesema kuwa timu hiyo kamwe haita muadhibu beki wake kisiki, Juma Said Nyoso kufuatia tukio lake la kumpiga shabiki mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba uliyofanyika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoka siku ya Jumatatu ya Januari 22, mwaka 2018.
Klabu ya Kagera Sugar kupitia kwa Mratibu wake, Mohamed Husein amesema kuwa timu hiyo kamwe haita muadhibu beki wake kisiki, Juma Said Nyoso kufuatia tukio lake la kumpiga shabiki mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba uliyofanyika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoka siku ya Jumatatu ya Januari 22, mwaka 2018.
Mratibu huyo, Husein ameyasema hayo kupitia mtandao wa michezo wa Shaffi dauda, Kagera Sugar haitochukua hatua zozote zile za kinidhamu dhidi ya beki wao Juma Nyoso ambaye ametoka Polisi kwa dhamana na tayari anaendelea na mazoezi.
“Jambo hili sisi tunaliangalia kwa macho mawili, kwanza tuweke wazi msimamo wetu, sisi hatutompa adhabu yoyote Nyoso kwa sababu yule shabiki alimkosea mchezaji wetu pamoja na Nyoso kuonekana kuwa na tabia ya ukorofi lakini kwa hili yule shabiki alimkosea na mimi nilishuhudia.”Inadaiwa shabiki huyo alitoa kauli chafu na za kuudhi kwa Nyoso pamoja na kumpigia kelele za vuvuzela kabla ya Nyoso kuamua kumpiga.
“Kumpulizia mtu vuvuzela kwenye sikio haikuwa sawa lakini wakati huo mchezaji ndio ametoka uwanjani kucheza, lakini shabiki huyo alikuwa akimshabulia Nyoso kwa matusi hata wakati mchezo unaendelea na wakati wa mapumziko bado aliendelea kumtukana sasa na yeye ni binadamu alighadhabika.”
“Shirikisho na polisi wao ndio wataona nini cha kufanya kwa hiyo sisi tunasubiri kuona polisi wataamua nini kama kwenda mahakamani au kumalizana nje ya mahakama sisi tupo tayari. Kijana ameachiwa kwa dhamana na sasa anaendelea na mazoezi na wenzie.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni