January 12, 2018 ni
siku ya kihistoria katika soka la nchi ya Saudi Arabia baada ya wanawake
nchini humo kuhudhuria mechi ya soka kwa mara ya kwanza.
Majira ya saa 2:00
usiku kwenye uwanja wa Mfalme Abdullah jijini Jedda, wanawake walikuwa
tayari uwanjani wakitazama mechi ya ligi kuu kati ya Al-Ahli dhidi ya
Al-Batin ambapo Al Ahli ilishinda mabao 5-0.
Prince Mohammad Bin Salman Al Saud
alitangaza kuwaruhusu wanawake kuingia uwanjani mwezi October 2017.
Hata hivyo wanawake wametengewa jukwaa lao “Family sections” ambapo
wataruhusiwa kukaa na familia zao bila kuchanganyikana na wanaume ambao
si wa familia zao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni