Jumamosi, 20 Januari 2018

Chelsea yainyanyasa Brighton ugenini EPL

Mabingwa watetezi wa ligi kuu England klabu ya Chelsea imefanikanikiwa chomoza na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Brighto.

Wakiwa ugenini Chelsea imepata ushindi wake kupitia kwa Willian dakika ya sita ya mchezo kabla ya Eden Hazard kufunga mabao mawili dakika ya tatu na 77 na Moses kutupia la mwisho na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa mabao 4-0.

Kufuatia mabao hayo Eden Hazardanafikisha jumla ya magoli (65) na pasi zilizochangia magoli (37)

Kwa matokeo hayo  Chelsea inasalia katika nafasi yake ileile ya tatu kwa kuwa na jumla ya pointi 50 sawa na Man United yenye alama 50, the Blues ikiwa mbele kwa mchezo mmoja ambapo imeshuka dimbani mara 24 wakati United inayoshika nafasi ya pili ikiteremka uwanjani mara 23 huku Liverpool wakiwa wa nne na alama zao 47.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni