
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA, imekipiga faini kituo cha runinga
cha Star TV ya jumla ya shilingi milioni 7.5 kwa makosa ya ukiukwaji wa
taratibu za kutangaza taarifa ya habari, inayotakiwa kulipwa ndani ya
siku 30 kuanzia leo.
Pia mamlaka hiyo imekiweka kituo hicho cha runinga kwenye uangalizi
maalum kwa muda wa miezi sita kuanzia leo, kutokana na kurusha taarifa
ya habari inayotajwa kuwa ya uchochezi.
Pia imekiadhibu kituo cha runinga cha Azam 2, kwa makosa ya kukiuka
maadili ya uandishi wa habari na kurusha habari zenye uchochezi kuhusu
uchaguzi wa madiwani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni