Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
amesema amesikitishwa na kifo cha msichana Marim Sandalu (17) aliyekuwa
na uvimbe begani.
Mariam
ambaye ni mkazi wa Masasi mkoani Mtwara, amefariki dunia leo alfajiri
akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI).
Binti
huyo ambaye alitakiwa kufanyiwa upasuaji Muhimbili mwaka mmoja uliopita
wakati huo uvimbe ukiwa bado mdogo, alitoweka baada ya kwenda katika
tiba za asili kabla ya kurejea hospitalini hapo Januari 3 mwaka huu,
baadaye kuhamishiwa katika taasisi hiyo.
Waziri Ummy amesema inasikitisha kwani msaada wa Watanzania haukuweza kuokoa maisha yake.
“Tutaongeza
jitihada zaidi kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuwahi
hospitalini kufanyiwa uchunguzi na kuzingatia maelekezo ya madaktari
wanayopewa ikiwamo kuanza matibabu mara moja na si kwenda kukaa nyumbani
na mgonjwa,” amesema Waziri Ummy ambaye hivi karibuni alimtembelea
Mariam hospitalini kumjulia hali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni