
Ijumaa, mvuvi huyu nchini Somalia anaonekana akiwa amembeba papa mkubwa ambaye alimvua baharini. Anaelekea katika soko la samaki la Hamarweyne karibu na mji mkuu wa Mogadishu.
Ijumaa, msichana akitembea karibu na
mabaki ya nyumba zilizoharibiwa na maporomo ya ardhi katika mtaa mmoja
mjini Kinshasa. Mafuriko huwatatiza sana wakazi wa mitaa ya mji huo mkuu
wa DRC kwa sababu nyumba nyingi zimejengwa kwenye maeneo tambarare na
mifumo ya kuondoa maji taka ni duni.
Siku hiyo pia, mwanamume nchini Sudan anaonekana akiondoka kwenye kiwanda cha kuoka mikate akiwa na mkate mjini Khartoum.
Bei ya mkate nchini Sudan imepanda
maradufu baada ya serikali kuondoa ruzuku. Polisi wamekuwa wakikabiliana
na wanafunzi wanaoandamana kulalamikia kupanda kwa bei.
Ijumaa pia, farasi hawa walionekana karibu na magofu ya mji wa Shahhat, Libya uliojengwa na Wagiriki na Warumi.
Katika taifa jirani la Algeria,
mwanamume anatazama mteremko ulio na theluji katika eneo la Ain Sefra,
Algeria katika Jangwa la Sahara Januari 7.
umatano, mteja jijini Naireobi
anaonekana akijaribu kufanya uamuzi wa kiatu atakachonunua miongoni mwa
viatu vilivyoundiwa China katika duka moja Januari 10.
Na nchini Morocco, mwanamume huyo
anaonekana kujawa na upweke akitembea ufukweni wakati wa futani mjini
Rabat Jumatatu. Taifa hilo limeshuhudia baridi kali siku za karibuni.
Na kasa hawa wadogo wanasubiri kuachiliwa huru katika bahari ya Atlantic nchini Benin...
. huku mwanaharakati mtetezi wa
uhifadhi akionekana akishiriki maonesho ya kuhifadhi kasa Siku ya Taifa
ya Kasa eneo la Grand-Popo nchini Benin.
Kasa wadogo hufa sana na ni wachache
sana hukomaa kufikia ukubwa wa kasa huyu aliyepigwa picha kwenye Bahari
ya Sham katika pwani ya Misri siku moja baadaye
Papa Tawadros II, kiongozi wa kanisa
la Coptic la Misri, naye anaonekana akiwaongoza waumini kwa ibada mkesha
wa Krismasi. Kinyume na Wakristo wengine ambao husherehekea Krismasi
mnamo 25 Desemba, kanisa la Coptic husherehekea sikukuu hiyo mnamo
tarehe 7 Januari. 
Kanisa la Kiothodoksi la Ethiopia pia husherehekea Krismasi tarehe 7UJanuari. Hapa, mwumini mmoja anaonekana akisoma Biblia akitumia mshumaa katika mji wa Lalibela kaskazini mwa nchi hiyo
Siku iliyotangulia, waumini
wanaaonekana wakitoka nje ya kanisa baada ya kushiriki maoni ya asubuhi
katika kanisa la Bete Amanuel, "Nyumba ya Emmanuel".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni