
Wapalestina
wamezima taa za krismasi kwenye mji mtakatifu wa Bethlehem alikozaliwa
Bwana Yesu, kupinga hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kuutambua
mji wa Yerusalem kama mji mkuu wa Israel.
Afisa
Habari wa Manispaa ya Bethelehem, Fady Ghattas amesema Mti wa Krismasi
ulioko kwenye kanisa la Bethlehem ambako wakristo huamini Bwana Yesu
alizaliwa, ulizimwa taa zake kwa amri ya Meya wa Manispaa hiyo.
Miji mingine iliyozimwa taa ni Ramallah ulio karibu na mahali alipozikwa kiongozi wa zamani wa Palestina Yasser Arafat.
Waarabu
na waislamu katika nchi za Mashariki ya kati wamepinga hatua ya Trump
ya kutangaza kutambua Yerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni