Jumamosi, 2 Desemba 2017

SportPesa waidhamini timu ya Bunge Mashindano ya Bunge Afrika Mashariki






Kampuni ya michezo ya kubashiri ijulikanayo kama SportPesa Limited imeidhamini timu ya mpira wa miguu na kikapu ya Bunge la Tanzania ambao wanatarajia kushiriki mashindano ya wabunge wa Afrika Mashariki mnamno Desemba 3, 2017 katika uwanja wa Taifa, Temeke Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za SportPesa zilizopo Masaki, Peninsula House Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji SportPesa Tanzania Mr. Tarimba Abbas alisema “Tulivyosikia kuwa haya mashindano ya wabunge wa Afrika Mashariki kwa mwaka huu yatafanyika nchini kwetu tuliona ni vyema kuwa wazalendo kwa kuidhamini timu ya mpira wa miguu na pete kwa kutoa vifaa mbalimbali vya michezo kama Jersey, bibs, soksi, pamoja na mipira. SportPesa ni kampuni ya kubashiri michezo mbalimbali ikiwa na kengo kuu la kukuza na kuendeleza sekta ya michezo nchini na ndiyo maana tulianza kwa kudhamini timu za mpira wa miguu za Simba, Yanga na Singida United.
“Mbali na hapo tutatoa tracksuits kwa ajili ya wabunge wote 160 wanaoshiriki katika mashindano hayo siku ya ufunguzi ambapo wabunge hao watafanya maandamano kutoka ukumbi wa PTA SABASABA kuelekea Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuanza michezo mbalimbali ya ufunguzi.”
“Tunapenda kuwapongeza na kuwatakia kila lakheri timu ya Bunge la Tanzania katika mashindano haya na tunaamini wataiwakilisha vizuri nchi yetu” alimaliza Mr. Tarimba


Naye Mwenyekiti wa klabu ya michezo ya wabunge Mh. William Ngeleja alianza kwa kusema “tunapenda kutanguliza shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa kwa ushirikiano wao waliouonyesha na kutusapoti katika kuhakikisha timu zetu za mipira wa miguu na pete zinapata vifaa vya michezo kama vile jezi, mipira na soksi.
“Tunatarajia kuanza rasmi mashindano yetu siku ya jumapili tarehe 03, desemba 2017 ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali za ufunguzi huo ikiwemo kukimbia, kuvuta kamba, mpira wa pete, mpira wa wavu pamoja ja mpira wa miguu”.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni