
SPIKA NDUGAI KWENDA KUMJULIA HALI LISSU- Spika wa Bunge Job Ndugai leo Ijumaa ameahidi kwenda kumjulia hali Mbunge Tundu Lissu hospitalini Nairobi au popote atakapokuwa baada ya Sikukuu ya Krismasi.
Ndugai pia amesema japo utaratibu wa kumsafirisha Lissu ulikuwa umepitia kushoto, Bunge lipo tayari kushirikiana na familia ya mgonjwa katika kukamilisha matibabu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Dodoma baada ya kupokea Barua ya Maulid Said Mtulia (CUF) na Dkt Godwin Aloyce Mollel ambao wamejiuzulu Ubunge. Mhe Spika amesema ameaiandikia Tume ya Uchaguzi ili iendelee na hatua nyingine.
(Picha kwa hisani ya Bunge)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni