Jumamosi, 30 Desemba 2017

Simba Kicheko Yaendeleza Kipigo kwa Ndanda Fc



 Simba inaendelea kuwa mbabe kwa Ndanda huu ukiwa ni mchezo wa saba mfululizo kwa Simba kushinda tangu Ndanda ipande daraja.

Simba imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Ndanda FC jioni ya leo Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Shujaa wa Simba leo alikuwa ni mshambuliaji na Nahodha wa sasa, John Raphael Bocco aliyefunga mabao yote hayo kipindi cha pili baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza.

Kwa ushindi huo, Simba inafikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 12, sawa na Azam FC walio nafasi ya pili kwa kuzidiwa wastani wa mabao.

Mabingwa watetezi Yanga SC wenye pointi 21 wanaendelea kushika nafasi ya tatu na wataendelea kukaa hapo hata wakishinda kesho dhidi ya Mbao FC mjini Mwanza sana washuke tu kama watatoa sare au kupoteza na Singida United washinde ugenini dhidi ya Njombe Mji FC.

Katika mchezo wa leo Uwanja wa Nangwanda, Bocco alifunga bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 52 akimalizia kona nzuri ya winga Shiza Kichuya kutoka upande wa kulia.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni