
Mshambuliaji wa klabu ya Real
Madrid, Mreno Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka
wa pili mfululizo usiku wa kuamkia leo.
Ronaldo amemshinda
mpinzani wake wa karibu Lionel Messi, katika tuzo hiyo na kuweza kuitwaa
kwa mara ya tano na kuwa sawa na Messi ambae pia ametwaa kwa mara
tano.Nyota wa Barcelona Lionel Messi, amepata nafasi ya pili huku mchezaji mahiri wa Psg ya nchi Ufaransa Neymar Jr,akiwa katika nafasi ya tatu
Msimu uliopita Ronaldo aliisaidia timu yake ya Real Madrid kutwaa ubingwa wa klabu bingwa barani Ulaya na ubingwa wa la Liga kwa mara ya kwanza toka toka mwaka 2012.
Ballon d'Or ni tuzo ambayo imekua ikitolewa na jarida la nchini Ufaransa toka mwaka 1956 na kura hupigwa na waandishi wa habari wapatao 173, duniani kote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni