Leo ni siku ya kimataifa ya kujitolea ambayo kila mwaka huwa Desemba 5, kauli mbiu mwaka huu ni "jitolee chukua hatua kwanza"
Ni kijana Hussain Salim mratibu wa miradi na matukio kutoka Rally Tanzania Society, taasisi isiyo ya kiserikali inayohusika na shughuli za kujitolea na inafanya kazi kwa karibu na Umoja wa Mataifa nchini humo katika kusongesha mbele malengo ya maendeleo endelevu SDGs.
Umoja wa Mataifa unasema maelfu ya wafanyakazi wake wa kujitolea kama kijana Hussein wana mchango mkubwa, katika kusaidia kufanikisha ajenda ya umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu ya 2030 lakini pia malengo ya jamii wanakojitolea. Hussein ana ujumbe
Hapa
ni nchini Sudan Kusini, Solomon Ayiko (kulia) mfanyakazi wa kujitolea
wa Umoja wa Mataifa akiwa kwenye doria na walinda amani kwenye njia
inayotumiwa na wanawake kusaka kuni, eneo ambalo ni hatari zaidi kwa
ukatili wa kingono na kijinsia.Pichani mkimbizi wa ndani akiwa
amemshikilia Solomon ili asiteleze wanapopita kwenye njia hii yenye maji
na madimbwi. (Picha:UNV/(Melanie Moore/ 2016)
Mbali ya mazingira wafanyakazi wa kujitolea wanashiriki katika
masuala mengine kadha wa kadha. Sudan kwa mfano kuna wafanyakazi zaidi
ya 200 wa kimataifa na kitaifa wanaojitolea kwenye mpango wa pamoja wa
Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur UNAMID,
na baadhi ya shughuli wanazofanya ni kujenga barabara, kuwawezesha
vijana, kuchagiza masuala ya haki za binadamu, kulinda watoto na
kuchangia katika juhudi za kuleta amani na maendeleo .Kwa mujibu wa Stuart J. Moran meneja wa mpango wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa Darfur bila mchango wao kibarua kingekuwa kigumu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni