Jumapili, 31 Desemba 2017

Kanisa Katoliki laitisha maandamano kutaka Rais aondoke madarakani Congo



Decemeber 31, 2017 makanisa 150 ya kanisa Katoliki yamewataka waumini wao kuitikia wito wa kuandamana  wakiwa na biblia mkononi ili kushinikiza kutekelezwa kwa makubaliano yaliyotiwa saini mwaka mmoja uliopita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Wasiwasi wa kukosekana utulivu katika nchi hiyo inayokabiliwa na mgogoro wa kisiasa kufuatia kanisa Katoliki lenye ushawishi Congo kuitisha maandamano ya amani yenye lengo la  kurejesha uthabiti nchini humo ikiwa ni pamoja na kumtaka Rais Joseph Kabila kuondoka madarakani.
Hakuna mtu yoyote kati ya Baraza la Maaskofu nchini humo au mwakilishi wa serikali ya mjini Vatican  ambaye amezungumzia lolote kuhusiana na maandamano hayo.





Gavana wa mji huo Andre Kimbuta amesema kuwa maandamano hayo yasiyo na kibali hayawezi kuendelea kwa maelezo kuwa mji huo hauna maafisa wa polisi wa kutosha kusimamia maandamano  ya leo.
Hata hivyo msemaji wa waratibu wa maandamano Leonie Kandolo amesisitiza kuwa licha ya kauli hiyo ya serikali maandamano yatafanyika na kuwa maafisa wa  polisi wanalazimika kutimiza wajibu wao kuwalinda raia na mali zao.
Waandaaji wa maanadamano  wametoa mwito kwa waumini kukusanyika baada ya misa ya asubuhi kwa ajili ya kushiriki maandamano hayo leo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni