Mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) imepuguza viwango vya gharama
za mawasilino ya simu kutoka shilingi 26.96 kwa dakika iliyokuwa
ikitozwa mwaka huu hadi shilingi 15.60 itakayoanza rasmi kutumiwa
mwakani.
Viwango hivyo vipya vitaanza kutumika Januari Mosi mwakani.Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Mhandisi James Kilaba amesema gharama hizo zitaendelea kupungua kila mwaka hadi zifikie shilingi mbili ifikapo mwaka 2022 hatua itakayochochea idadi ya watumiaji wa mawasiliano na hivyo kuongeza pato la watoa huduma na Taifa kwa jumla.
Wakati umuhimu wa huduma za mawasiliano ukizidi kuongezeka, gharama za
mwingiliano wa mitandao ya simu ambazo kwa sasa ni shilingi 26.96 kwa
dakika zinaonekana kuwa ni kikwazo kwa watumiaji wengi ambao wameitaka
TCRA kuzifuatili kampuni za simu zenye tabia ya kupandisha gharama za
vifurushi na aina nyinginezo kiholela na hivyo kuwaibia wateja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni