Jumapili, 31 Desemba 2017

Chonde Chonde 2018 tubadilike la sivyo ......- Guterres



Heri ya mwaka wapendwa marafiki kote duniani! Mwaka huu unapoanza sitoi ombi bali natoa angalizo!
Hiyo ni sehemu ya salamu za mwaka mpya za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa wakazi wa dunia hii wakati mwaka mpya wa 2018 unapoanza.
Bwana Guterres anasema msingi wake wa kutoa angalizo ni kwamba ombi alilotoa la amani wakati mwaka 2017 unaanza halikuzaa matunda
 Kwa bahati mbaya kwa namna mbalimbali hali imeenda kinyume . Machafuko yamezidi kuongezeka na hatari mpya zimezuka. Hamasa ya dunia kuhusu silaha za nyukliaimefikia kiwango cha juu zaidi tangu  wakati wa vitabaridi. Mabadiliko ya Tabianchi yanaenda kasi kuliko sisi.Ukosefu wa usawa unaongezeka"


"Mabadiliko ya Tabianchi yanaenda kasi kuliko sisi. Ukosefu wa usawa unaongezeka. Tunaona ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.Utaifa na ubaguzi nao unaongezeka ."
Hivyo Katibu Mkuu anatoa ombi…

 "Nawaomba viongozi kila mahali kulifanya azimio la mwaka mpya.Tupunguze mapengo. Kuondoa mgawanyiko. Turudishe uaminifu kwa kuwaleta watu pamoja tukiwa na lengo moja.Umoja ndio njia.Musthakbali wetu unategemea hili. Nawatakia amani na afya njema kwa mwaka 2018. Asante."

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni