imba
SC na kocha wake mkuu Joseph Omog (pichani), wameamua kwa pamoja
kuvunja mkataba baina yao kwa makubaliano maalum yanayozingatia maslahi
ya pande zote mbili.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Simba imeeleza kuwa timu hiyo itakuwa chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma na kumtakia kila la kheri kocha Omog.
"Klabu inamshukuru kocha Omog na inamtakia kila la kheri kwenye maisha yake nje ya Simba".
Pia klabu hiyo imewaomba radhi mashabiki wa Simba kwa matokeo ya mchezo wa jana ambao Simba ilitupwa nje ya michuano ya #ASFC na Green Warriors katika mchezo wa raundi ya pili.
"Kwa niaba ya uongozi, benchi la ufundi na wachezaji.tutumie nafasi hii kuwaomba radhi sana Wanachama na washabiki wetu kwa matokeo ya jana, sote tumeumia ila ndio mchezo wa mpira ulivyo, na tuwaombe muwe watulivu katika kipindi hiki ili tufikie malengo yetu," Imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni