Jumapili, 26 Novemba 2017

Wapenzi wafunga ndoa hospitalini alipolazwa baba wa Bi Harusi akisubiri kifo



Binti mmoja wa Kimarekani Vieneese, 27 na mchumba wake Douglas, 30, Stanton wa California, Marekani hivi karibuni wamekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuamua kufunga ndoa hospitalini.
Wawili hao walifikia uamuzi huo baada ya baba mzazi wa bibi harusi Preston Rolan, 64, kuwa amelezwa katika hospitali ya San Francisco Medical Center ya Chuo Kikuu cha California, huku ripoti za madaktari zikieleza kuwa baba huyo amebakiza wiki chache tu kuishi kutokana na ugonjwa wa saratani ya damu ‘Leukemia’.
Inaeleza kuwa wachumba hao walipanga harusi yao ifanyike April 2018 lakini baada ya kupokea taarifa hiyo ya madaktari, ndipo walipoamua kuifanya November 2017, ili tu baba huto ahudhurie na kshuhudia bini yake anavyoolewa.
Harusi hiyo ilihudhuriwa na wauguzi na madaktari, pamoja na ndugu jamaa na marafiki wa familia hizo.





Image result for Viennese and Douglas Stanton wedding

 Image result for Viennese and Douglas Stanton wedding

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni