Alhamisi, 30 Novemba 2017

Ukata waleta zahma kwa wakimbizi wa Burundi huko Tanzania:UNHCR




Maelfu ya wakimbizi wa Burundi wanaishi katikia hali mbaya kwenye makambi nchini Tanzania kwa sababu ya ukata wa fedha limesema leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Leah Mushi na taarifa kamili
(TAARIFA YA LEAH)
Kwa mujibu wa shirika hilo upungufu wa fedha za kufadhili miradi ya kuwasaidia wakimbizi hao imesababisha wengi kuendelea kuishi katika mahema ya dharura wengine tangu miaka miwili iliyopita walipowasili kwenye kambi hizo za Nyarugusu na Nduta mkoni Kigoma Magharibi mwa Tanzania.
UNHCR inasema madhila yamezidishwa na kuingia kwa wimbi kubwa la wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kufuatia machafuko ya karibuni. Sandrine Nyaribagiza ni miongoni mwa maelfu ya wakimbizi wanaoishi kambini hapo..

 Hivi sasa UNHCR na washirika wake wameanza kuwahamishia wakimbizi hao kwenye makazi ya mpito na kusaidia mradi utakaowawezesha kujenga makazi yao .  Makazi hayo ya mpito ni bora zaidi lakini yanapatikana tu kwa wakimbizi waliowasili karibuni. Patrick Mutai ni afisa wa makazi wa UNHCR kwenye kambi hizo.


"Punde wanapohamia kwenye makazi hayo na kutulia taratibu wanaweza kuanza kufyatua matofali ya matope na kuanza ujenzi ili kuboresha makazi yao ya kudumu au ya muda, hivyo inapunguza muda wa wakimbizi hawa kuishi katika mahema na makazi ya dharura."
Ingawa makazi hayo yanatoa matumaini, UNHCR inasema fedha zaidi za  ufadhili zinahitajika ili kuwasaidia maelfu ya wakimbizi ambao bado wanaishi kwenye hali mbaya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni