Alhamisi, 30 Novemba 2017

Simba kufanya usajili mwingine



Simba ina mpango wa kumsajili mtu ambaye atamaliza tatizo la umaliziaji.

Kocha Msaidizi wa Simba, Djuma Masoud amesema mpango wao msimu huu ni kuhakikisha wanafanya usajili bora.

Dirisha dogo la usajili lilifunguliwa hivi karibuni na linatarajiwa kufungwa Desemba 15, mwaka huu.
Djuma alisema kuwa wanahitaji wachezaji wanne wa nguvu ambao ni kipa, beki wa kati, winga pamoja na straika.

Masoud amesema kuwa licha ya uhitaji huo wa wachezaji hao, hata hivyo mchezaji ambaye wanamuhitaji zaidi ni mshambuliaji.

Alisema sifa ambazo wanataka mshambuliaji huyo wanayemhitaji awe nazo ni awe anajua kuzitumia vizuri nafasi za kufunga ambazo atakuwa anazipata uwanjani, awe na uwezo mkubwa wa kupambana na mabeki wa timu pinzani lakini pia awe anajua kutafuta nafasi za kufunga.

“Tunataka kuhakikisha tunafanya vizuri msimu huu na kuvunja utawala wa Yanga, lakini pia ukiachana na ligi kuu pia tunakabiliwa na mashindano wa kimataifa kwa hiyo tunataka kuwa na mshambuliaji wenye uwezo mkubwa na mwenye sifa hizo.

“Tunaendelea na harakati zetu na muda si mrefu naamini tutampata lakini pia wachezaji hao wengine ambao tunawahitaji,” alisema Masoud ambaye ni raia wa Burundi aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni akichukua mikoba ya Mganda, Jackson Mayanja. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni