
Baada ya zoezi refu la uchaguzi nchini Kenya hatimaye nchi hiyo imefanikiwa kumrudisha Rais Uhuru Kenyatta Madarakani kwa muhula wa pili.
Kenyatta wakati anaapishwa leo jumanne tarehe 28 Novemba 2017, kwenye viwanja vya Kasarani amewashukuru Wakenya wote kwa kumrudisha madarakani na kuahidi kuwatumikia bila ubaguzi.
Moja ya ahadi aliyoitoa ni kupunguza gaharama za matumizi ya umeme nyakati za usiku ili kuongeza chachu ya ukuaji wa uchumi wa taifa hilo.
Kenyatta amesema Wakenya wanapaswa kuishi kama ndugu na kuacha siasa za uhasama kwani hazitasaidia kukuza uchumi wa nchi yao.
Kwa upande wa Mahakama Rais Kenyatta amesema atakaa na jopo la majaji kuangalia namna ya kuharakisha upatikanaji wa haki kwa haraka zaidi ili kuondoa msongamano wa kesi kwenye mahakama zao.
Ushirikiano wa Kenya na nchi nyingine za Afrika kibiashara:
Moja ya vitu ambavyo Rais Kenyatta ameviahidi ni kuimarisha mahusiano na nchi za Afrika kwa kuruhusu watu watakaotaka kufanya biashara nchini humo kupatiwa visa.
Rais Kenyatta amesema kuanzia sasa Mwafrika yoyote kutoka taifa lolote anayetaka kuingia Kenya atapatiwa visa wakati anaingia kwenye maeneo yote ya kuingilia kuanzia kwenye viwanja vya ndege na mipakani yaani kwa maana hiyo mtu yeyote ataweza kuingia nchini humo ili mradi tu awe na kitambulisho cha uraia.
“Tutaendelea kuimarisha uhusiano wetu wa kiuchumi, Kila mwafrika atakayetembelea Kenya atapata Visa atakapoingia kwenye maeneo ya viwanja vya ndege na mipakani, hii yote ili kukuza uchumi wa Afrika yetu… Naahidi nitawahudumia Wanaafrika Mashariki kama Wakenya.“amesema Kenyatta.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache zilizopita tangu Rwanda nayo itangaze hivyo ingawaje Rwanda ilitangaza kwa kila raia atakayeingia nchini humo.
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo nchini Tanzania, Zitto Kabwe ameonekana kuguswa na ahadi hiyo ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter amempongeza Kenyatta kwa hatua hiyo.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni