
Spika wa bunge la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu .
Spika wa bunge Jacob Mudenda alisema kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na
amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko ya amani ya mamlaka
kulingana na chombo cha habari cha Reuters.Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake.
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Reuters, Spika wa bunge amesema kuwa kiongozi mpya atawekwa madarakani siku ya Jumatano.

Awali bwana Mugabe alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung'atuka mamlakani wiki hii.
Amekuwa mamlakani tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake 1980.
Bwana Mugabe ameshinda uchaguzi wa urais mara kadhaa lakini katika kipindi cha miaka 15 iliopita shughuli hiyo imekumbwa na ghasia dhidi ya wapinzani wake
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni