Mtetezi wa Umoja wa Mataifa wa waathirika wa ukatili wa kingono Jane Connors, amesema kundi hilo linachohitaji ni ujenzi wa maisha mapya baada ya kuumizwa na ukatili huo ambao ni kinyume na ubinadamu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani, kutoa tathimini yake ya ziara ya majuma mawili aliyoifanya nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati sambamba na Katibu Mkuu Antonio Guterres, ziara iliyomkutanisha na wahanga na wadau wa ukomeshwaji wa ukatili wa kingono, Bi Connors amesema licha ya msaada wa kisaikolojia, chakula na dawa kubwa ni.
'Kwangu, niliona kuna mengi zaidi ya kufanya hususani elimu. Na nilibaini hatari kubwa ni kukosa elimu, sio tu kwa sababu kusoma hulinda, lakini pia kwasababau wale ambao hawana elimu wako hatarini zaidi ,hawana taarifa.Kwahiyo nafikiri hili ni eneo ambalo lahitaji uangalifu zaidi.''
Mtetezi huyo wa wahanga wa ukatili wa kingono ambaye ni wa kwaza kuteuliwa na Katibu Mkuu, kushika nafasi hiyo, amesema atafanya kazi zaidi katika maeneo yenye watetezi ambao wanafanya kazi na ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika nchi nne zenye idadi kubwa ya visa hivyo ambazo ni Haiti (MINUJUSTH), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, (MONUSCO) Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, MINUSCA na Sudan Kusini UNMISS.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni