
Kikosi cha kijeshi cha Misri
kimeanza mashambulio dhidi ya ngome za wanamgambo wanaodhaniwa ndio
waliosababisha vifo vya watu wapatao 235 baada ya kuwashambulia katika
eneo la rasi ya Sinai wakati walipokuwa wanatoka msikitini.
Waathiriwa
wengi wa shambulio hilo lililofanywa na wanamgambo walikuwa ni
wanawake, wanaume na watoto pamoja na maafisa wa jeshi waliokuwa
wakitoka msikitini .Serikali ya Misri imetangaza siku tatu za maombolezi kufuatia mauaji hayo
Rais Abdel-Fattah al-Sisi ameahidi kuchukua hatua kali dhidi ya wanamgambo hao.
Eneo hilo la Sinai hukumbwa na mashambulio ya mara kwa mara yanayofanywa na wanamgambo wanaopinga serikali ya Misri, na msikiti uliolengwa ni maarufu sana na waumini wa madhehebu ya kisufi na watu wa kabila la -Sawarka wanaosemekana kuunga mkono kikamilifu serikali ya rais rais Abdel-Fattah al-Sisi .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni