
erikali ya awamu ya tano leo imetimiza miaka miwili tangu kuingia madarakani huku ikijanasibu kupata mafanikio makubwa kwenye nyanja mbalimbali za uchumi, pamoja na kudai kufanikisha kurejesha nidhamu na uwajibikaji kwa watumishi wa umma.
Msemaji wa Serikali Dkt. HASSAN ABBAS akitoa tathmini ya miaka miwili ya Utawala wa Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli, amebainisha kuwa licha ya nidhamu kwa watumishi wa umma, kuongezeka wigo wa ukusanyaji wa kodi ya mapato, udhibiti wa vyeti feki na watumishi hewa vimesaidia serikali katika kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma ambazo ilikuwa ikitumia.
Dk Abbas akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam amesema katika watumishi hewa 20,000 serikali imeweza kuokoa zaidi ya shilingi bilion 238, wakati katika udhibiti wa vyeti feki watumishi 12,000 waliondolewa na hivyo serikali kuokoa zaidi ya shilingi bilion 142.9.
Channel ten ilitaka kujua hatua ambazo zimechukuliwa na serikali ya awamu ya tano katika kumsaidia mkulima kuongeza tija ikiwemo kuondokana na jembe la mkono.
Akielezea kuhusiana na changamoto iliyojitokeza kwa Serikali ya awamu ya Tano wakati wa utawala wake, Dk HASSAN ABBAS ambaye pia ni mkurugenzi wa idara ya habari maelezo amebainisha kwa sasa ni kuongezeka kwa maadui hasa wale waliokuwa wamezoea kupata fedha kwa njia za mkato, baada ya mianya yote kuzibwa.
Novemba tano mwaka 2015 Rais John Pombe Magufuli pamoja na makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan waliapishwa rasmi kushika uongozi wa taifa hili kwa kipindi cha miaka mitano hadi mwaka 2020.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni