Mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara umemalizika katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea kwa wenyeji Majimaji FC kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stand United.
Baada ya bao lililofungwa na Massele Boniventure dakika ya 51 na kuipatia ushindi huo wa kwanza msimu huu timu ya Majimaji inapanda hadi nafasi ya 10 kutoka nafasi ya 14 iliyokuwapo hapo hawali huku Stand United ikisalia nafasi ya 15.
Ligi hiyo itaendelea tena wikiendi hii kwa vinara wa VPL, Simba SC, Yanga SC na Azam FC kujitupa viwanjani.
Msimamo wa ligi baada ya mchezo wa leo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni