 |
Mhe. Julius Kambarage Nyerere(1961-1962)
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Waziri Mkuu wa Kwanza wa Serikali ya
Tanganyika Huru kuanzia tarehe 9 Desemba, 1961 hadi tarehe 22 Januari,
1962 alipojiuzulu na kumwachia Mheshimiwa Rashidi Mfaume Kawawa wadhifa
huo ili yeye aende kuiimarisha TANU mikoani. |
|
|
 |
Mhe. Rashid Mfaume Kawawa (1962 1972-1977)
Waziri Mkuu wa Pili wa Serikali ya Tanganyika kuanzia tarehe 22
Januari, 1962 akipokea nafasi hiyo kutoka kwa Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere. |
|
|
 |
Mhe. Edward Moringe Sokoine (1977-1980 1983-1984)
Waziri Mkuu wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliwahi kuwa
Waziri Mkuu mara mbili, tangu tarehe 13 Februari, 1977 hadi 7 Novemba,
1980 na mara ya pili kuanzia tarehe 24 Februari, 1983 hadi tarehe 12
Aprili, 1984 alipofariki kutokana na ajali ya gari. |
|
|
 |
Mhe. Cleopa David Msuya (1980-1983 1994-1995)
Waziri Mkuu wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea nafasi
hiyo kutoka kwa Mheshimiwa Edward M. Sokoine. Aliwahi kushika wadhifa
wa Waziri Mkuu mara mbili. Mara ya kwanza ni kuanzia tarehe 7 Novemba,
1980 hadi tarehe 24 Februari, 1983. Mara ya pili ilikuwa ni tarehe 5
Desemba, 1994 hadi tarehe 28 Novemba, 1995 huku akishika pia wadhifa wa
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa sasa,
ameshastaafu siasa ingawa bado anashika nyadhifa mbalimbali za uongozi
katika Taasisi mbalimbali za Jamii. |
|
|
 |
Mhe. Salim Ahmed Salim (1984-1985)
Waziri Mkuu wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea
nafasi hiyo kutoka kwa Mheshimiwa Edward M. Sokoine ambaye alifariki kwa
ajali ya gari mnamo tarehe 12 Aprili, 1984. Ni mwanadiplomasia wa siku
nyingi kuanzia miaka ya 1960. Alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kuanzia
tarehe 24 Aprili, 1984 hadi tarehe 5 Novemba, 1985 akifuatiwa na
Mheshimiwa Joseph Sinde Warioba. |
|
|
 |
Mhe. Joseph Sinde Warioba (1985-1990)
Waziri Mkuu wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea
nafasi hiyo kutoka kwa Mheshimiwa Dkt. Salim Ahmed Salim. Ni
mwanasheria, mwanasiasa maarufu, Jaji wa siku nyingi. Alikuwa Waziri
Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kuanzia tarehe 5 Novemba 1985 hadi tarehe 9 Novemba 1990 akifuatiwa na
Mheshimiwa John Samuel Malecela. |
|
|
 |
Mhe. John Samuel Malecela (1990-1994)
Waziri Mkuu wa Saba wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea
nafasi hiyo kutoka kwa Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba. Alikuwa
Waziri Mkuu wa Tanzania kuanzia tarehe 9 Novemba, 1990 hadi tarehe 5
Desemba, 1994 akifuatiwa na Mheshimiwa Fredrick Tluway Sumaye. |
|
|
 |
Mhe. Frederick Tluway Sumaye (1995-December,2005)
Waziri Mkuu wa Nane wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea
nafasi hiyo kutoka kwa Mheshimiwa John Samuel Malecela. Alikuwa Waziri
Mkuu wa Tanzania kuanzia tarehe 28 Novemba, 1995 hadi tarehe 29 Desemba,
2005 akifuatiwa na Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa. |
|
|
 |
Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (2005-2008)
Waziri Mkuu wa Tisa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea
nafasi hiyo kutoka kwa Mheshimiwa Fredrick Tluway Sumaye. Alikuwa Waziri
Mkuu wa Tanzania kuanzia tarehe 30 Desemba, 2005 hadi tarehe 7
Februari, 2008 alipojiuzulu na hatimaye kuvunjwa kwa Baraza la
Mawaziri.Alikifuatiwa na Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda.
|
 |
Mhe. Mizengo Peter Pinda (2008-2015)
Waziri Mkuu wa Kumi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea
nafasi hiyo kutoka kwa Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa . Aliteuliwa
tarehe 7 February, 2008 na baadae alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania baada
ya kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia
tarehe 9 Februari, 2008 hadi tarehe 5 Novemba 2015. Akifuatiwa na
Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa
|
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni