Klabu ya Sevilla imethibitisha kuwa mkufunzi wake amepatikana na ugonjwa wa saratani baada ya timu hiyo kutoka nyuma na kupata sare ya 3-3 dhidi ya Liverpool.
Wachezaji wa Sevilla wakishangilia na kocha wao baada ya kusawazisha goli katika dakika za mwisho
Vyombo vya habari vinasema kuwa Eduardo Berizzo ambaye anaugua
saratani ya tezi dume aliwaelezea wachezaji wake kuhusu habari hiyo
katika wakati wa mapumziko katika uwanja wa Estadio Ramon Sanchez
Pizjuan.Wachezaji wa Sevilla walimkimbilia Berizzo baada ya Guido Pizarro kufunga katika dakika za lala salama ili kusawazisha.
Taarifa ya klabu hiyo imemtakia mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 48 kupona kwa haraka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni