Mpanda milima mashuhuri duniani kwa kutumia baiskeli ,Juanito Oiarzabal
na wenzake wawili wamekamilisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa
kutumia saa 31 ndani ya siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru.
Juanito Oiarzabal akiwa katika kilele cha Uhuru baada ya kufika huko huku akiendesha baiskeli
Safari ya wageni hawa, Juanito na wenzake wawili , Eduardo Pascuaz na
Ramon Abecia kupanda Mlima mkubwa kulikoyote barani Afrika na wapili
kwa urefu duniani kwa kutumia Baiskeli ilianzia kupitia lango la Kilema.

Juanito Oiarzabal ambaye amepata ulemavu wa kukatika vidole kutokana na
barafu katika Milima mbalimbali aliyopanda amesema changamoto
aliyokutana nayo wakati wa kupanda mlima ni kuzoea hali ya hewa ya mlima
ambayo imekuwa ikibadilika kila wakati.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni