
Novemba
2, 2017, Chama cha ACT Wazalendo kilipokea wito toka kwa Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) wa kuwataka Wajumbe wote wa
Kamati Kuu ya ACT Wazalendo wafike Kituo cha Makosa ya Fedha (Financial
Crime Unit) kilichopo Maeneo ya Kamata, Kariakoo Jijini Dar es salaaam
kwa ajili ya mahojiano siku ya Jumatatu, Novemba 6, 2017.
Ikumbukwe
kuwa wito huu unakuja baada ya Kiongozi wa Chama, ndugu Kabwe Z.
Ruyagwa Zitto kuhojiwa katika kituo hicho kwa takribani masaa matatu
Oktoba 31, 2017 kutokana na Taarifa ya Chama kuhusu Kusinyaa kwa Uchumi.
Uamuzi huu wa kuihoji Kamati Kuu nzima unashangaza sana kwa sababu mbili:
i.
Kamati Kuu ni chombo cha kitaifa cha Chama chenye mamlaka ya kufanya
maamuzi kwa mujibu wa katiba ya ACT Wazalendo kama chombo na si kama
mjumbe mmoja mmoja.
ii. Jeshi la Polisi halina madaraka ya kushughulikia wala kuingilia maamuzi halali ya vyombo (organs) katika vyama vya siasa.
Tangu
tuzindue kampeni zetu katika kata ya Kijichi, Jeshi la Polisi limefanya
maamuzi ya kushikilia au kuhitaji kuwahoji viongozi wetu, maamuzi
ambayo kwa namna moja au nyingine yanaathiri kampeni zetu. Kwa maamuzi
haya ya Jeshi la Polisi, ni wiki sasa inakatika viongozi wetu
wakilazimika kusalia jijini Dar es salaam kusubiri kuhojiwa na Polisi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni