


Tume ya uchaguzi nchini Kenya imekadiria kwamba idadi ya wapiga waliojitokeza katika marejeleo ya uchaguzi wa urais imefikia asilimia 33.4
Hiyo ikiwa ni chini kwa asilimia 8 ikilinganishwa na uchaguzi wa mwezi Agosti ikionyesha kuwa mamilioni ya Wakenya walifuata wito wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga kususia uchaguzi huo.
Upigaji kura umesitishwa hadi siku ya Jumamosi katika kaunti nne ambapo wafuasi wa upinzani walizozana na maafisa wa polisi.
Gavana wa kaunti ya Kisumu aliambia BBC kwamba waandamanaji wawili uawa kutokna ana majereha ya risasi. Waandishi wanasema kuwa idadi hiyo ya waliojitokeza, kupiga kura inazua maswalai kuhusu uchagzi huo.
VIjana watumia nyuki kuzuia upigaji kura Kenya
Vijana hao walibeba mzinga wa nyuki katika shula ya msingi ya Matsakha na kuwalazimu maafisa wa IEBC kuwaita maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Malava.
Wapiga kura wachache walilazimika kuondoka katika lango la kituo hicho cha kupiga kura kwa hofu ya kushambuliwa na nyuki.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo la Malava Anne Muli aliongiza operesheni ya kukabiliana na nyuki hao.
Awali maafisa wa polisi walikuwa wamewakamata baadhi ya vijana katika eneo la Matsakha na Shilongo kwa kujaribu kuharibu uchaguzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni