
Mkuu wa mkoa Morogoro ametoa hadi Oktoba mwaka huu kwa wafugaji kukamilisha zoezi la kupiga chapa mifugo na wenye mifugo isiyo na chapa watachukuliwa hatua.
Kufuatia kusuasua kwa baadhi ya wafugaji kupiga chapa mifugo yao Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Kebwe Stephen Kebwe ametoa hadi Oktoba 30 mwaka huu kwa wafugaji kuhakikisha mifugo yao imepigwa chapa na kutambuliwa vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaokiuka ikiwemo adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya shilingi Milioni kumi.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi katika maeneo mbalimbali,Mkuu huyo wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen,Kebwe amesema muda wa nyongeza uliotolewa kukamilisha upigaji chapa mifugo uko mbioni kumalizika lakini bado mwitikio ni mdogo huku baadhi wakigomea kabisa zoezi hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni