Jumapili, 29 Oktoba 2017

Mawakili watatu watimuliwa nchini



Serikali ya nchini Tanzania imewafukuza mawakili watatu wa Afrika Kusini waliokamatwa wiki hii Jijini Dar es Salaam wakituhumiwa kwa kuchochea mapenzi ya jinsia moja.

Mawakili hao waliofukuzwa ni wale waliokuwa miongoni mwa watu 13 waliokamatwa katika hoteli moja mjini Dar es Salaam wakijiandaa kufanya mkutano wa kujadili iwapo wakabiliane na uamuzi wa serikali ya Tanzania kuzuia utoaji wa baadhi ya huduma za afya au la kwa mujibu wa mawakili hao.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa jana wakati akizungumza na wanahabari  amewaambia kuwa kabla ya mawakili hao kukamatwa kwamba walikuwa wakichochea mapenzi ya jinsia moja.

Mapema mwaka huu, serikali ilipiga marufuku baadhi ya kliniki za kibinafsi kutotoa huduma za ugonjwa wa HIV na ukimwi ikisema zilikuwa zikukuza mapenzi ya jinsia moja ambayo ni haramu nchini Tanzania.

Hata hivyo kukamatwa kwa Mawakili hao kunatokea kufuatia hotuba ya mwezi Septemba iliotolewa na aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya Dkt. Hamis Kingwangala (kwa sasa ni Waziri wa Maliasili) ambaye aliapa mbele ya bunge kukabiliana na makundi yoyote yanayounga mkono wapenzi wa jinsia moja nchini. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni