Jumanne, 10 Oktoba 2017

LEO NI SIKU YA AFYA YA AKILI DUNIANI .Msongo wa mawazo hugharimu dola trilioni 1 kila mwaka- WHO


Leo ni siku ya afya ya akili duniani ambapo maudhui ni afya njema ya akili pahala pa kazi ili kuongeza tija.
Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema kiwewe na msongo wa mawazo husababisha kupungua kwa tija na hivyo kuleta hasara ya dola trilioni moja kila mwaka duniani.
Takwimu za WHO zinaonyesha kwamba zaidi ya watu milioni 300 ulimwenguni wanakabiliwa na kiwewe na msongo wa mawazo miongoni mwao wakiwa ni wafanyakazi.
WHO inasema afya njema ya akili pahala pa kazi ni jambo muhimu kwa kuzingatia kuwa kipindi kikubwa cha utu uzima mtu hukitumia akiwa kazini.
Uzoefu unaonyesha kuwa waajiri wanaozingatia mazingira bora ya afya ya akili ya wafanyakazi wao na hata kuwasaidia wale wenye matatizo hupata tija kubwa kwani mazingira yasiyo rafiki kwa afya njema ya mwili na akili hupunguza tija.
Hivyo WHO imesihi mataifa kutumia siku ya leo kuangazia na kuhamasisha umuhimu wa afya ya akili ili kuimarisha afya hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni