Mchekeshaji mkongwe Bongo, Joti hatimaye ameamua kuachana na utani wa
kudai anaoa na kuamua kufanya kweli kwa kudhihirisha yupo serious
kidogo kwa jambo la mahusiano kwa kutarajia kuvuta jiko hivi karibuni.
Joti ambaye anafahamika kwa kufanya matangazo mengi ikiwemo ya
kufunga ndoa , aliambatana na watu wake wa karibu katika sendoff
yake iliyofanyika siku ya jana( Alhamisi) akiwa na mchekeshaji Seki.
Mchekeshaji huyo mwenye dili kibao town anatarajia kufunga ndoa
rasmi hivi karibuni na atakuwa ameingia kwenye orodha ya mastaa wa
Bongo waliopo katika ndoa kama Babuu wa Kitaa, Mx Carter, Kenedy The
Remedy, Professa Jay, ZamaradI Mketema na Frola Mbasha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni