Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein akihutubia waandishi wa habari. Picha: UN Photo/Jean-Marc Ferré
Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad
Al Hussein amesema ana wasiwasi mkubwa kuhusiana na ghasia
zinazoendelea huko Catalonia nchini Hispania kufuatia kura ya wakazi wa
jimbo hilo kutaka kujitenga na nchi hiyo.Kamishna Zeid amenukuliwa akitaka mamlaka nchini humo kuhakikisha uchunguzi wa kina na huru ufanyika ili kubaini wahusika.
Amesema wakati wowote polisi ni lazima wawe makini wanapotumia nguvu dhidi ya raia na wafanye hivyo pale ambapo ni lazima.
Ameongeza kuwa anaamini hali ya sasa inaweza kusuluhishwa kupitia mazungumzo ya kisiasa huku uhuru wa kidemokrasia ukizingitiwa.
Kamishna Zeid amehitimisha taarifa yake akitoa wito kwa serikali ya Hispania kukubali bila kuchelewa maombi ya wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuzuru nchi hiyo kujionea hali halisi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni