Jumatano, 20 Septemba 2017

Kikosi kipo tayari sasa dhidi ya Mbao FC – Mayanja



 Timu ya Simba SC tayari ipo mkoani Mwanza kujiwinda na mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara hapo kesho siku ya Ahalimisi  dhidi ya Mbao FC.


Kupitia mtandao wakijamii wa klabu hiyo umeeleza kuwa wachezaji wa Simba SC wameshuka dimba la CCM Kirumba kufanya mazoezi kabla ya kukabiliana na Mbao FC.
Kikosi cha Simba leo kimefanya mazoezi yake ya mwisho kujiandaa na mchezo dhidi ya Mbao FC katika uwanja wa CCM Kirumba.
Akiongea na Simba News Kocha, Jackson Mayanja amesema “leo tunafanya maandalizi ya mwisho kabisa, kikosi kipo tayari kabisa kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Mbao FC, ni timu nzuri na yenye ushindani wake”.
“Tutaingia uwanjani tukiwa tunajua aina ya timu ambayo tunakwenda kupambana nayo. Mashabiki waje kwa wingi kwa ajili ya kuisapoti timu yao katika kutafuta matokeo mazuri kwenye mchezo wetu wa kwanza kwenye uwanja wa ugenini katika msimu huu”.
Kikosi cha Simba kesho kitashuka dimbani kucheza mchezo wake wa kwanza katika uwanja wa ugenini, ambapo utapigwa majira ya saa 10:00 jioni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni