Alhamisi, 24 Agosti 2017

AJALI: Daladala imegonga Treni asubuhi hii mjini Morogoro



 WANAFUNZI wawili  wamefariki dunia nawengine29 kujeruhiwa  kufuatia ajali mbaya ya basi la abiria aina ya Coaster lililobeba wanafunzi na raia kugonga treni katika eneo la TANESCO, Morogoro Mjini.

Taarifa za awali zimeeleza kuwa ajali hiyo imetokea leo alfajiri ambapo Coaster lilikuwa limebeba wanafunzi wengi wa Shule ya Sekondari ya Kayenzi waliokuwa wakienda shuleni pamoja na raia wachache lilipokatiza kwenye njia ya treni na kuligonga.

Imeelezwa pia kuwa treni liliibuiruza Coaster hiyo kwa umbali wa mita 30 kabla ya kusimama hivyo kusababisha vifo hivyo na majeruhi.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni