
Maafisa kutoka Hifadhi ya Taifa ya
Garamba nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamesema kuwa Tembo 45
wameuawa tangu mwanzo wa mwaka huu.
Maafisa hao wanasema endapo
uhalifu huo utaendelea kukithiri, Tembo huenda wakapotea kabisa katika
mbuga hiyo, ambayo ni moja ya maeneo yaliyo na tembo wengi zaidi barani
afrika. Ripoti zinasema Ndovu hao huuawa na makundi ya waasi nchini DRC, wapiganaji wa kundi la waasi wa LRA kutoka Uganda, na waasi wa Sudan Kusini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni