Jumamosi, 8 Julai 2017

Watu milioni 30 wanakabiliwa na njaa- FAO




Mtoto anayeugua utapiamlo nchini Somalia katika kambi ya Salamey Idale.(Picha:UNICEF/Rich)
Dunia inakabiliwa na janga kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miongo kadhaa, huku watu milioni 30 katika nchi nne wakikabiliwa na uhaba wa chakula na wengi wakiwa katka hatari ya ukame limesema Shirika la kilimo na chakula duniani FAO.
Akizungumza katika kongamano la FAO huko Roma, Italia Naibu mkurugenzi mkuu wa mipango, FAO Daniel Gustafson amesema nchi hizo nne ambazo ni Kasakazini Mashariki mwa Nigeria, Somalia, Sudan Kusini na Yemen bado hali ni tete licha ya hatua zilizopigwa katika kukabiliana na ukame.
Bwana Gustafson ameongeza kwamba ushirikiano wa Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa kutoa misaada imesaidia pakubwa lakini akaonya kwamba bado safari ni ndefu katika kuhakikisha hakuna janga la njaa lingine mwaka huu huku akitaja kitu kinachofanana katika nchi hizi nne ni…

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni